Nyuma kwenye Habari
Taarifa19 Julai 2026

ZOEZI LA KUJISAJILI UANACHAMA WA CCM TAWI LA INDIA

Ndugu Wanachama, Viongozi na Wananchi wote, Napenda kuwataarifu kuwa zoezi la usajili wa wanachama wa CCM Diaspora – India kupitia tovuti rasmi ya Tawi limeanza rasmi kuanzia leo, tarehe 19 Julai, 2026. Hatua hii inalenga kurahisisha usajili wa wanachama wapya, kuboresha utunzaji wa taarifa za wanachama, na kuimarisha ushiriki wa Watanzania wanaoishi nchini India katika shughuli za Chama Cha Mapinduzi kupitia mfumo wa kidijitali. Tunawaomba viongozi wote wa Tawi, viongozi wa Jumuiya za CCM, hususan UVCCM, pamoja na wanachama wote, kushiriki kikamilifu katika kuhamasisha Watanzania wanaoishi India kujisajili kupitia tovuti rasmi ya Tawi. Ushirikiano wenu utasaidia kuhakikisha kuwa zoezi hili linafanyika kwa ufanisi na kufikia malengo yaliyokusudiwa. Tunawahimiza wanachama wote ambao bado hawajajisajili kutumia fursa hii kufanya usajili wao mapema kupitia tovuti rasmi ya Tawi. Aidha kwa wale ambao hawana Namba ya kielectronic au hawajawi kuwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi, na wanahitaji kujiunga na Chama Cha Mapinduzi, wawasiliane na viongozi husika ili wawawezeshe kuweza kujisajili uanachama wa Chama Cha Mapinduzi. Kwa pamoja tuendelee kuijenga CCM imara na yenye mshikamano ndani ya Diaspora ya India. Imetolewa na: IS-HAKA RASHID HADID KATIBU MKUU- CHAMA CHA MAPINDUZI INDIA
ZOEZI LA KUJISAJILI UANACHAMA WA CCM TAWI LA INDIA